Timu kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali imewasili mkoani Kigoma kuanza kazi ya tathmini ya mali za wananchi watakaoguswa na ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma.
Timu hiyo, ikiongozwa na Mthamini Kiongozi James Mark Mwanakatwe, inaendelea na uthamini wa maeneo katika wilaya za Tabora Mjini, Uyui, Urambo, Kaliua, Uvinza na Kigoma.
Mwanakatwe amesema hadi sasa wamekamilisha uthamini wa vipande 52 vya ardhi, vikiwemo eneo la daraja la Mto Malagarasi lenye urefu wa kilomita tatu, na kwa sasa wanaendelea na kipande cha kilomita 72.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates