Kupitia taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake Katibu Mkuu amesema kimbunga hicho kimeacha athari kubwa nchini Jamaica, Cuba na Bahamas  huku mafuriko makubwa yakiripotiwa pia nchini Haiti na Jamhuri ya Dominika.

Taarifa hiyo imesema  Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa “ana wasiwasi mkubwa” na amesimama kwa mshikamano na serikali pamoja na wananchi walioathiriwa na Kimbunga Melissa.”

Katibu Mkuu pia “Amewapa pole za familia zote za waliopoteza wapendwa wao katika kimbunga hicho na anawatakia majeruhi wote ahuweni ya haraka.”

Jumuiya za Visiwa vya Karibea zilikabiliana na Kimbunga Melissa, ambacho tayari ni dhoruba ya Aina ya 4 na kinatarajiwa kuimarika zaidi. (picha ya faili)

© UNICEF/Roger LeMoyne

Jumuiya za Visiwa vya Karibea zilikabiliana na Kimbunga Melissa, ambacho tayari ni dhoruba ya Aina ya 4 na kinatarajiwa kuimarika zaidi. (picha ya faili)

UN tayari inasaidia waathirika

Umoja wa Mataifa umeanza kutoa msaada wa dharura, huku timu zake zikiwa tayari mashinani kusaidia kutathmini madhara na kusaidia juhudi za kitaifa. Pia, umetoa dola milioni nne kwa kila nchi mmoja Haiti na Cuba kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) ili kusaidia jamii kujiandaa na kupunguza athari za kimbunga hicho.

Taarifa hiyo imesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutuma wahudumu wa ziada kwa muda mfupi na kuzindua maombi ya misaada ya dharura kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu yatakayosababishwa na kimbunga hicho.”
Kimbunga Melissa ni miongoni mwa vimbunga vyenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba Karibea, na kinatishia maisha ya mamilioni ya watu kutokana na mafuriko, uharibifu na kufurushwa katika makazi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *