
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kuwa watu wasiopungua 7,455 wamekimbia imji wa El fasher magharibi mwa Sudan katika muda wa siku moja kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
Katika muda wa wa siku tatu watu 33,485 wameukimbia mji wa El Fasher kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa RSF.
Mamlaka za Sudan na taasisi za kimataifa na za Umoja wa Mataifa kwa siku kadhaa sasa zimekituhumu kikosi cha RSF kuwa kimefanya mauaji ya umati na kukiuka haki za binadamu dhidi ya raia katika mji wa El Fasher ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela, kuwakamata raia na kuwalazimisha kuhama, ambapo kundi hilo lilianza kuushambulia mji huo siku ya Jumapili baada ya kuuzingira kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza katika taarifa yake kuwaa watu zaidi ya 7,455 wanakadiriwa kuhama makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea huko El-Fasher na kwamba ripoti zinaonyesha kuwa watu 33,485 wamelazimika kuhama makazi yao kati ya tarehe 26 hadi jana Jumanne.
Juzi Jumatatu, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilibainisha kuwa idadi ya raia waliolazimia kuacha makazi yao katika mji wa El Fasher kuanzia Oktoba 26 hadi 27 imefikia 26,030.
Makadirio yasiyo rasmi yanaonyesha kuwa mji wa El Fasher ulikuwa na jamii ya watu wasiopungua laki tano huku wengine karibu milioni moja walikuwa tayari wameuhama mji huo katika miaka ya karibuni kabla ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuushambulia mji huo.