
Wizara ya Mambo ya Nje imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu machafuko yanayoendelea katika jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, na kulaani mauaji ya raia na uharibifu wa miundombinu katika mji wa El-Fasher.
Katika taarifa yake Jumanne wiki hii Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Esmaeil Baqaei amebainisha kutiwa wasiwasi na mapigano hayo ya silaha, na kulaani “uharibifu wa miundombinu na mauaji ya watu wasio na hatia” katika mji ulioathiriwa na vita wa El Fasher.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ameonya kuhusu “harakati hatari zinazolenga kuigawanya tena Sudan,” na kusisitiza kuwa ipo haja ya kuheshimiwa mamlaka ya kitaifa na umoja wa ardhi ya nchi hiyo.