
Watanzania waliotimiza masharti ya kupiga kuraa leo wanaelekea katika vituo vya kupigia kuura kwa ajili ya kumchagua Rais, Wabunge na madiwani katika uchaguzi uliosusiwa na chaama kikuu cha upinzani cha CHADEMA.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (INEC) imetangaza kuwa, maandalizi yote kwa ajili ya uchaguzi wa leo yamekamilika.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, karibu Watanzania milioni 38 wametimiza masharti ya kupiga.
Wagombea kutoka vyama 17 vinavyoshiriki uchaguzi huo jana walitupa karata zao za mwisho kwa wapiga kura katika kampeni za lala saalama kabla ya hatma yao kuamuliwa leo wakati wapiga kura wenyewe wanapoelekeaa katika vituo vya kupigia kura.
Rais aliyeko madarakani Mama Samia Suluhu Hassan anayegombea kwa tiketi ya chama tawala cha mapinduzi CCM anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi hasa kutokana na kutokuweko mpinzani mwenye nguvu.
Chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesusia uchaguzi huo kutokana na kile kilichosema kutofanyika marekebisho ya maaana katika sheria za uchaguzi likiwemo suala zima la Katiba mpya.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA, Tundu Lissu ambaye chama chake kimesusia uchaguzi kikidai kufanyike mageuzi kwenye mfumo mzima wa uchaguzi anashikiliwa kizuizini akikabiliwa na kesi kadhaa.
Ama uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na kile kinachotazamwa kama ukosoaji wa mitandaoni ambako wananchi wa ndani na wale wa nje ya nchi wamekuwa wakitumia majukwaa hayo kwa ajili ya kujadili na kuhamasisha maandamano.
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limeonya kuhusu hatua yoyote itakayoweza kutibua uchaguzi huo na kusema kwamba linakusudia kufanya doria karibu maeneo yote ya nchi.
Wangalizi wametakiwa kutoingilia kazi za tume, na wafuate sheria na muongozo wa uangalizi. Zoezi hili linakuja baada ya kampeni za uchaguzi zilizodumu kwa siku 61.