Licha ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA kutangaza kuwa hakuna ongezeko lolote la urutubishaji urani nchini Iran, lakini wakati huo huo amedai kuwa kumeonaka harakati mpya katika vituo vya nyuklia vya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, Rafael Grossi, jana Jumatano jioni alifanyiwa mahojiano na shirika la habari la Associated Press na kusema kuwa, hadhani kwamba kwa hivi sasa Iran inaongeza urutubishaji urani. 

Ameendelea kudai kwamba harakati mpya zimeonekana hivi karibuni katika vituo vya nyuklia vya Iran na alionesha picha za satelaiti za chuo kimoja cha Marekani kutilia nguvu madai yake hayo. 

Katika sehemu nyingine ya mahojiani hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomoki IAEA amesema kuwa, IAEA hivi sasa iko katika mazungumzo mazuri na Iran na inajaribu kupanua wigo wa ukaguzi wa vituo vya nyuklia ingawa bado haijaruhusiwa kukagua vituo vyote. 

Amesisitiza tena kwa kusema kuwa, hana ushahidi wowote wa kuonesha kuweko ongezeko la urutubishaji urani nchini Iran. Grossi pia amesema kuwa mazungumzo yanayoendelea kati ya IAEA na Iran ni muhimu.

Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba mpango wake wa nyuklia ni wa uzalishaji wa nishati na ni kwa ajili ya kufaidika na teknolojia hiyo ya kisasa kwa masuala ya kiraia kama vile matibabu na matumizi ya kilimo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki aidha amesema: “Tunarejea polepole. Kwa sasa hatukagui vituo vilivyoshambuliwa vya huko Natanz, Isfahan na Fordow. Lakini nataka kusema kuwa, mazungumzo kati yetu na Iran yanaendelea vizuri.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *