
Mashtaka mapya ya unyanyasaji na ukatili uliofanywa na jeshi la Mali yameibuka. Matukio hayo yanaripotiwa kutokea Oktoba 23 katika mkoa wa Ségou. Askari, wakiungwa mkono na wawindaji wa jadi wa Dozo, wanashukiwa kuwaua raia zaidi ya thelathini karibu na eneo la Markala, katikati mwa nchi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wengi wa waathiriwa walikuwa wafugaji waliokuja baada ya kuvuka Mto Niger na mifugo yao katika mkoa wa Ségou katikati mwa Mali. Tukio hili la kila mwaka huwaleta pamoja wakazi wa eneo hilo kuelezea furaha na mshikamano wao na wafugaji hao wanaorejea kutoka uhamiaji wao wa msimu, lakini sherehe hizo zilihitimishwa kwa umwagaji damu.
Mashahidi waliowasiliana na RFI wanaweka wazi kuhusu matukio hayo. Wakati wafugani walikuwa wakiendelea kuvuka mto huo Alhamisi asubuhi, Oktoba 23, kundi la wanajeshi wa Mali, wakisaidiwa na wawindaji wa Dozo, walivamia ukingo wa mto.
Milio ya risasi ilisikika
Kundi hilo lilifyatua risasi mara moja bila onyo. “Waliwapiga risasi wanaume na mifugo,” ameeleza mchungaji ambaye hakutaka kutajwa jina, akiongeza, “Nilinusurika kwa sababu nilikuwa nimefika upande wa pili wa mto.”
Akiwa na kiwewe, mwanamume mwingine alisimulia kumuona kaka yake akianguka chini baada ya kupigwa ya wanajeshi kumpiga risas. Hasira inaongezeka ndani ya jamii ya wafugaji, kwani mamlaka iliarifiwa kuhusu sherehe hiyo na watu kuvuka mto kwenda upande wa pili.
Kulingana na hesabu iliyotolewa na vyanzo vya ndani, raia 32 waliuawa. Wakazi wanaoishi kando ya mto walieleza kwamba alasiri, wanajeshi wa Mali walirudi na kuwazika waathiriwa katika makaburi mawili ya pamoja. Katika hatua hii, jeshi wala serikali ya Mali haijazungumza chochote.