Ni mustakabali gani unaosubiri Sahara Magharibi? Swali hili litakuwa katikati ya kura muhimu leo Alhamisi hii, Oktoba 30, katika Umoja wa Mataifa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapitisha azimio linaloongeza muda MINURSO, ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliopewa jukumu tangu mwaka 1991 la kuandaa kura ya maoni kuhusu kujitawala katika eneo hili lenye mgogoro. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Lakini mwaka huu, nakala zilizowasilishwa na Marekani zimerekebishwa kwa kiasi kikubwa. Zinapendekeza kufanya mpango wa uhuru wa Morocco wa mwaka 2007 kuwa mwanzo wa kuanza tena kwa mazungumzo. Maendeleo haya makubwa ya kidiplomasia, yanayoungwa mkono haswa na Washington na Paris, na ni ushindi mkubwa wa kisiasa kwa Rabat dhidi ya Polisario Front.

Mazungumzo ya kidiplomasia yalikuwa makali mnamo Oktoba 29, siku moja kabla ya kupiga kura kuhusu Sahara Magharibi. Na sababu: nakala ya azimio lililopendekezwa na Marekani yanaashiria mabadiliko halisi. Nakala hiyo inapendekeza kutumia mpango wa uhuru wa Morocco wa mwaka 2007 kama msingi wa kuanzisha tena mazungumzo. Msimamo huu unaipainufaisha Rabat, kwani ungeunga mkono uhuru wa Morocco juu ya eneo linalozozaniwa, ukivunja msimamo wa kihistoria wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala hili.

Suala jingine muhimu katika kura hii ni muda wa mamlaka ya MINURSO. Utawala wa Trump umetaka kuongezwa kwa miezi mitatu pekee, si mwaka mmoja kwa kawaida. Hata hivyo, ukikabiliwa na upinzani, makubaliano yalifikiwa kwa ajili ya kuongezwa kwa miezi sita. Lengo ni kuruhusu muda wa mazungumzo chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa na kuepuka kuacha suala hilo mikononi mwa Marekani pekee.

Morocco yaonekana kuungwa mkono

Nakal zitakazopigwa kura zinaonyesha mabadiliko katika makubaliano ya kimataifa yanayopendelea msimamo wa Morocco katika miaka ya hivi karibuni. Kimsingi, Baraza la Usalama linaonekana kupendelea azimio hili, lakini baadhi ya mambo yasiyojulikana yanabaki, hasa kura za China na Urusi, ambazo zinashikilia kura ya turufu na zinaweza kushawishi matokeo. Beijing na Moscow zinadumisha uhusiano wa karibu na Algeria, ambayo ni mfuasi wa Polisario Front na inayopendelea uhuru wa eneo hili la jangwani.

Nyuma ya pazia, mazungumzo yanaendelea kurekebisha maneno ya rasimu ya awali ya Marekani, kuanzisha upya dhana ya kujitawala, na kuhakikisha kupitishwa kwa azimio hilo na wengi kati ya wanachama kumi na watano wa Baraza la Usalama la moja w Mataifa. Mazungumzo haya ni makali zaidi ikizingatiwa kwamba Algeria ni mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kulingana na vyanzo vyetu, nakala ya pili iliyopendekezwa na Marekani tayari imekataliwa na Algiers, ambayo kwa hivyo haitarajiwi kushiriki katika kura hiyo, kama ilivyokuwa mwaka jana, anaripoti mwandishi wetu huko Casablanca, François Hume-Ferkatadji.

Nakala iliyowasilishwa kwa kura hiyo inaonyesha mabadiliko katika makubaliano ya kimataifa yanayoipendelea Morocco, ikiwa ni pamoja na ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Mbali na Marekani, Ufaransa na Uingereza tayari zimeonyesha kuunga mkono mpango wa uhuru.

Ili azimio hilo lipitishwe, ni lazima lipate kura tisa kati ya wanachama kumi na watano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: wanachama watano wa kudumu—China, Ufaransa, Urusi, Uingereza, na Marekani—pamoja na wanachama kumi waliochaguliwa kwa mihula miwili ya miaka miwili, ikiwa ni pamoja na Algeria, Korea Kusini, Denmark, Ugiriki, Guyana, Pakistan, Panama, Sierra Leone, Slovenia, na Somalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *