Kremlin imewatuliza nyoyo baadhi ya viongozi wa dunia leo Alhamisi, Oktoba 30, kuhusiana na matangazo yake ya hivi karibuni kuhusu majaribio ya chombo cha majini kisicho na nahodha cha Urusi na kombora lenye uwezo wa nyuklia, ikisisitiza kwamba haya hayakuwa “majaribio ya nyuklia” kwa maana halisi, kufuatia uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Kuhusu majaribio ya Poseidon na Burevestnik (majina ya vyombo vya majini visivyo na nahodha vya Urusi chini na kombora), tunatumai kwamba Rais Trump alifahamishwa ipasavyo. Hili haliwezi kuchukuliwa kuwa jaribio la nyuklia,” msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema.

Tangazo hili linakuja baada ya uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuanza tena majaribio ya silaha za nyuklia.

Zaidi ya makombora na ndege zisizo na rubani 700 zilirushwa na Urusi jana usiku, kulingana na Jeshi la Anga la Ukraine. Msichana wa miaka 7 alifariki Vinnytsia, watu watano waliuawa katika eneo la Donetsk, na wawili huko Zaporizhzhia.

“Mtoto mmoja amefariki kufuatia shambulio la anga la Urusi huko Vinnytsia”, idara ya huduma za dharura ya serikali ya Ukraine imetangaza. “Alifariki hospitalini kutokana na majeraha aliyoyapata.

Watu wengine wanne walijeruhiwa,” idara ya huduma za dharura ya serikali ya Ukraine iliripoti siku ya Alhamisi. “Wazima moto tayari wamezima moto katika moja ya maeneo, huku shughuli zikiendelea katikamaeneo mengine,” taarifa hiyo imeongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *