
Rais wa Brazil Lula ametangaza siku ya Jumanne, Novemba 4, kwamba operesheni ya polisi dhidi ya kundi la wahalifu huko Rio de Janeiro iliyowaua watu 121 wiki iliyopita ilikuwa “mauaji ya halaiki” na akatoa wito wa uchunguzi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kulikuwa na mauaji ya halaiki, na nadhani ni muhimu kuchunguza mazingira ambayo vifo hivyo vilitokea,” Luiz Inacio Lula da Silva amesema huko Belém (kaskazini mwa Brazili) wakati wa mahojiano na mashirika ya habari ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na AFP.
Baada ya operesheni mbaya zaidi ya polisi katika historia ya Brazil, ambayo ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 121, Rais Lula alitoa wito Jumatano “kutowaweka hatarini” raia na mapambano dhidi ya uhalifu uliopangwa.
Katikati ya vilio na hasira, wakazi walipata miili kadhaa siku ya Jumatano ya wiki iliyopita kufuatia uvamizi wa siku ya Jumanne dhidi ya kundi linalofanya biashara haramu ya dawa za kulevya katika Complexo da Penha na Complexo do Alemão, majengo makubwa kaskazini mwa Rio.
Wakati Brazil ikijiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa viongozi wa dunia huko Belém, katika Amazon, kwa ajili ya mkutano wa tabia nchi COP30, wa Umoja wa Mataifa, operesheni hii inakumbusha nguvu ya uhalifu uliopangwa nchini na inaibua maswali mazito kuhusu mbinu za polisi katika vitongoji maskini zaidi.