
Maafisa wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels wamesema mazungumzo yaliofanyika jana Jumanne mjini humo yalimalizika bila maelewano na kuendelea usiku kucha.
Mapema leo, msemaji wa Denmark ambayo kwasasa inashikilia urais wa zamu, amesema wanaamini kuwa wana msingi wa makubaliano ya kisiasa.
Pia amesema wanatarajia kuhitimisha rasmi makubaliano watakaporejea kukutana tena baada ya saa chache.
EU yasisitiza kuhusu umuhimu wa mazungumzo ya hali ya hewa
Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza umuhimu wa mazungumzo hayo, ambayo yanakuja kabla ya mkutano huo wa Brazil.
Waziri wa mazingira wa Ufaransa Monique Barbut ameonya kwamba kuhudhuria mkutano huo bila makubaliano yoyote, kutasababisha kile alichokiita janga kwa Umoja wa Ulaya.