Kupitia taarifa kwenye mtandao wa Telegram, jeshi hilo limesema kuwa mabaki hayo yalikuwa ya Itay Chen mwenye umri wa miaka 19, mwanajeshi mwenye uraia pacha wa Marekani na Israel ambaye pia alikuwa na uraia wa Ujerumani.

Jeshi hilo pia limesema Chen aliuawa wakati wa mapigano katika eneo la Kibbutz Nir Oz, na kwamba kifo chake kilithibitishwa rasmi mnamo Machi 10, 2024.

Chen alikuwa mateka wa mwisho mwenye uraia wa Marekani na Israel aliyesalia katika Ukanda wa Gaza.

Mabaki ya Chen yalikabidhiwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na baadaye kusafirishwa kwa taasisi ya ukaguzi wa kimatibabu nchini Israel kwa utambuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *