
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas katika Ukanda wa Gaza imesema kuwa haiwezakani kutumwa kikosi chakijeshicha kigeni katika eneo hilo ambacho kitahudumu kama mbadala wa jeshi vamizi la Israel.
Mousa Abu Marzouk Afisa wa ngazi ya juu wa Hamas amesema katika mahojiano na televisheni ya al Jazira kwamba harakati hiyo haiwezi kukubali kikosi chochote cha kijeshi ili kuchukua nafasi ya jeshi ghasibu la utawala wa Kizayuni huko Gaza.
Abu Marzouk ameeleza haya baada ya Marekani baada ya Marekani kusambaza rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloamuru kuanzishwa kwa “kikosi cha muda cha kimataifa” katika Ukanda wa Gaza kwa muda usiopungua miaka miwili, huku Wapalestina wakitahadharisha juu ya hatari ya uingiliaji kati wa nchi ajinabi huko Gaza.
Tovu ya Axios ya nchini Marekani imeeleza kuwa kikosi cha kimataifa kwa jina la International Stabilization Force (ISF) kitaundwa na Marekani, Uturuki, Qatar na Misri nchi nne zilizosimamia mazungumzo yaliyofanikisha usitishaji vita kati ya utawala wa Israel na harakati ya Hamas mwezi uliopita.
Makubaliano hayo yanalenga kutekeleza awamu ya kwanza ya mpango wa vipengele 20 wa Donald Trump ambao Rais wa Marekani anadai kuwa umedhamiria kuhitimisha vita vya miaka miwili na mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel katika kUkanda wa Gaza.
Marzouk amesema itakuwa vigumu kwa Baraza la Usalama kupasisha mradi wa kuanzisha kikosi cha kimaifata huko Gaza kwa mujibu wa mpango wa Marekani.
Ameongeza kuwa si Marekani wala Israel inayotaka kuasisiwa kikosi hicho kupitia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.