Grossi ameliambia gazeti hilo  kwamba wakati shirika la IAEA likiwa tayari limefanya duru kadhaa za ukaguzi nchini Iran tangu uhasama na Israel mnamo mwezi Juni, halijaruhusiwa kufikia vinuu vya nyuklia kama vile Fordow, Natanz na Isfahan, ambazo zilishambuliwa na Marekani .

Iran yapaswa kuzingatia yaliomo katika makubaliano ya nyuklia

Grossi pia amesema wakati shirika hilo linajaribu kushirikiana na Iran kwa maelewano, nchi hiyo bado inahitajika kuzingatia yaliomo.

Kwa upande wake, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmaeil Baghaei, amesema Grossi anafahamu kikamilifu hali ya amani ya mpango wa nyuklia wa Iran na hapaswi kutoa maoni aliyoyataja kutokuwa na msingi juu yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *