Na Abu Bilaal Abdulrazaq bn Bello bn Oare

“Nyoka anayejitolea kukuimbia anafanya hivyo kukupima anaweza kukugonga vipi kwa ukaribu.” 

Huu ni msemo wa zamani wa Kiafrika ambao unaonya kuhusu kuamini watu bila kutafakari — kwa watu ambao wanaamini kila kitu kinachosemwa na mataifa ya nje, wanaweza kupoteza busara yao na uhuru. 

Kwa bahati mbaya, hii ndiyo njia inayoonekana kufuatwa na Nigeria baada ya tamko la hivi karibuni la Rais wa Marekani Donald Trump, kuieleza Nigeria kama nchi ambayo wana jambo nayo na kudai, bila kutoa ushahidi wowote, kwamba Wakristo nchini Nigeria wanakabiliwa na mauaji ya halaiki. 

Trump alionya kuwa kama serikali ya Nigeria “itaendelea kuruhusu kuuawa kwa Wakristo, Marekani itasitisha misaada kwa Nigeria mara moja, na inaweza kuvamia nchi hiyo ambayo inatia aibu kwa sasa, ’ ili kuangamiza kabisa magaidi wa Kiislamu ambao wanatekeleza ukatili mbaya sana”. 

Matamshi yake yamezidisha kutoaminiana miongoni mwa jamii mbalimbali, ambazo kwa miaka mingi,imekuwa ikijitahidi kuponya vidonda vya tofauti za kidini. 

Kutoka Iraq hadi Libya, Afghanistan hadi Somalia, uvamizi wa Marekani umesababisha uharibifu kwa mataifa — kutatiza, kugawanya, na kuyaacha yakiwa katika hali mbaya kuliko yalivyokuwa. 

Yote haya kwa kisingizio cha kuleta demokrasia, uhuru, au wasiwasi kuhusu hali za watu. Lakini pale mambo yanapotulia, ule unaosemekana kuwa uhuru unasababisha vurugu, na ukosefu usalama wa muda mrefu.

Kufikiria kwamba itakuwa tofauti kwa Nigeria kwa “wasiwasi huo” ni kubeza matukio ya kihistoria. 

Hatari zaidi, huenda ikasababisha raia wa Nigeria kukabiliana wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya kidini, raia dhidi ya raia, wakati ambapo umoja na maelewano yanahitajika zaidi nchini humo.

Unafiki huu unakuwa mkubwa wakati mtu anapoangalia nje ya mipaka ya Nigeria. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *