Zohran Mamdani mwenye umri wa miaka 34 amechaguliwa meya wa jiji la New York nchini Marekani, Mamdan Mmarekani mwenye asili ya India lakini aliyezaliwa Uganda kabla ya kuhamia Marekani akiwa na miaka saba, amewashinda Andrew Cuomo mwenye umri wa miaka 67  mwanasiasa wa muda mrefu na Mrepublican Curtis Sliwa

Zohran Mamdani mwenye asili ya Afrika aliyezaliwa barani Afrika hususan nchini Uganda anaandika historia mpya kwa kuwa muislaumu wa kwanza kuwa meya wa jiji maarufu la New York nchini Marekani. Mwanadipolamasia huyo wa kishoshalist.

Pia amekuwa meya mwenye umri mdogo wa miaka 34 kuliongoza jiji hilo ambalo huchukuliwa kama makao makuu ya dunia.

Akizungumza katika hotuba yake ya kwanza baada ya kushinda Zohran Mamdan ameuambia umati wa mashabiki wake kuwa kuchaguliwa kwake kunaleta nuru mpya katika jiji la New York ambalo amesema limekuwa katika giza kutokana na utawala wa Rais Donald Trump

“Ni wakati huu wa giza la kisiasa la kisiasa ambapo New York itapata mwanga, hapa tunaamini katika kusimama kidete kwa ajili ya wale tunaowapenda, hata hivyo ikiwa kuna mtu anayeweza kuonyesha nafasi yake kwa ajili ya taifa lililosalitiwa na Donald Trump ni hapa hapa ambapo pia palipomsaidia kupanda.”

Aliongeza kuwa “kama kuna njia za kumtetemesha muimla ni kuyaondoa mazingira yaliyofamfanya yeye kupata mamlaka, New York litasalia kuwa jiji la wahamiaji, jiji ambalo lilijengwa na wahamiaji, kupewa nguvu na wahamiaji kwa usiku huu likiongozwa na mhamiaji”

Zaidi ya Wamarekani milioni 2 walipiga kura katika mpambano huu ambayo ilikuwa idadi  kubwa kabisa ya wapiga kura waliojitokeza ndani ya kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Mamdani aufananisha ushindi wake kama nuru kwa wanyonge

Mamdani ameufananisha ushindi wake kama faraja aliyoitoa kwa wafanyakazi wa daraja la chini kabisa na wale wa daraja la kati huku akiahidii mabadiliko ya hali iliyopo.

Marekani | New York 2025 | Zohran Mamdani
Meya Mteule wa jiji la New York Zohran Mamdani akiwa na mke wake.Picha: Yuki Iwamura/AP Photo/picture alliance

Kuibuka kwa Mamdani bila kutarajiwa kunatoa uthibitisho kwa Wademokrats ambao wamekuwa wakihimiza chama hicho kukubali wagombea wa mrengo wa kuleta mageuzi kwa ajili ya raia wa daraja la chini na kati.

Katika sherehe ya ushindi katika eneo la Brooklyn, wafuasi wa Mamdani walishangilia na kukumbatiana baada ya Mamlaka  ya Jiji kutangaza ushindi wake.

Mabango ya kampeni yalipeperushwa angani,huku  mtu mmoja akiruka juu juu na bendera rasmi ya Jiji la New York, na muziki wa mwanamuziki maarufu Bad Bunny ulisikika kuoitia vipaza sauti hapa na pale.

Hata hivyo hivyo mjini Manhattan mgombea mwenza Andrew Cuomo katika hotuba yake ya kukubali kushindwa,  akaameonya kwamba ushindi wa Mamdani unaweza kuipeleka New York katika hatari huku akiwaahidi wafuasi wake kwamba anakwenda kujianda kwa ajili ya kurudi katika mpambano.

Sasa Mamdani atapaswa kuongoza Jiji kuu zaidi nchini Marekani na kutekeleza ahadi zake kubwa ambazo baadhi ya wachunguzi wanasema zinaonekana kutowezekana kutekelezwa ikiwa ni pamoja na malezi ya watoto bila gharama, kuanzishwa kwa kitengo maalum cha usalama wa raia na kupiga marufuku maduka ya vyakula yanayomilikiwa na serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *