Haya ni kulingana na makadirio yaliyotolewa na shirika la habari la NBC nchini humo.
Ushindi kwa Mamdani unaupatia mji huo meya wake wa kwanza Muislamu na kiongozi mwenye umri mdogo zaidi kwa muda mrefu.
Kinyang’anyiro hicho kilikuwa kimewapatanisha Mamdani mwenye umri wa miaka 34 ambaye alishinda mchujo wa chama cha Democratic mapema mwaka huu na Andrew Cuomo ambaye ni amegombea wadhfa huo kama mgombea huru pamoja na Curtis Sliwa wa chama cha Republican.
Fedha za New York kuzuiliwa na Trump
Rais Donald Trump na wanasiasa wa chama cha Republican wamekuwa wakimtaja Mamdani kama sura ya chama kipya chenye itikadi kali cha Democratic.
Trump pia alitishia kuuchukua mji wa New York na kuzuia fedha za mji huo iwapo Mamdani angeshinda na pia amkamate mbunge wa mji huo ambaye alizaliwa Uganda ila ni raia wa Marekani na amrudishe nchini Uganda.
Wapiga kura mjini New York wameweka rekodi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kumchagua meya wa mji huo.
Iwapo Cuomo angeshinda kiti hicho atakuwa amerudi kwa kishindo kikubwa cha kisiasa miaka minne baada ya kuachia ngazi kama gavana, kufuatia msururu wa madai ya udhalilishaji wa kingono yaliyomkabili.
Iwapo Sliwa naye angeshinda basi mji mkubwa zaidi nchini Marekani utakuwa chini ya mrepublican wakati ambapo wakaazi wa New York walikuwa wanamtafuta kiongozi ambaye atampelekea Rais Donald Trump kutoingilia masuala ya mji huo.
Trump na wanasiasa wa chama cha Republican wamekuwa wakimtaja Mamdani kama sura ya chama kipya chenye itikadi kali cha Democratic.
Trump pia alitishia kuuchukua mji wa New York iwapo Mamdani angeshinda na pia amkamate mbunge wa mji huo ambaye alizaliwa Uganda ila ni raia wa Marekani na amrudishe nchini Uganda.
Trump amemuunga mkono Cuomo katika uchaguzi huo akisema Mamdani ataleta kile alichokiita “janga” na akawataka wafuasi wa Sliwa kumpigia kura gavana huyo wa zamani wa New York.
Wamarekani waujibu utawala wa Trump
Kwengineko Mdemocrat Abigail Spanberger ameshinda kiti cha ugavana wa Virginia kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Hiki ni kinyang’anyiro cha kwanza ambacho ni kama kipimo cha jinsi Wamarekani wanavyomjibu Donald Trump na utawala wake uliokosolewa pakubwa ambao ndio uko katika mwezi wake wa tisa.
Spanberger mwenye umri wa miaka 46 ni mbunge wa zamani katika bunge la congress na afisa wa zamani wa shirika la upelelezi Marekani, CIA atakuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama gavana wa Virginia baada ya kumshinda kwa urahisi mrepublican Winsome Earle-Sears.
Wakati huo huo chama cha Democratic kimejinyakulia pia wadhfa wa ugavana katika mji wa New Jersey baada ya Mikkie Sherrill kuibuka mshindi.