Afisa wa jeshi huko Bundibugyo Albert Kaliruga, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Muganzi aliongoza kundi linalotaka kuchukua silaha ili kuanzisha uasi wa kikabila, lakini kwamba limerudishwa nyuma na vikosi vya usalama.

Wapiganaji 20 wauawa na 15 kukamatwa

Kaligura amesema Muganzi alizingirwa kwenye maficho yake huko Kakuka, Bundibugyo hapo jana na kuuawa pamoja na zaidi ya wapiganaji wake 20, huku wengine 15 wakikamatwa.

Kaligura ameongeza kusema Muganzi alikuwa akitumia madhabahu yake ya kitamaduni kuwasajili na kuwafunza wapiganaji wake pamoja na kutumia dawa za mitishamba na imani za kishirikina ili kuwalinda wakati wa vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *