Wakati wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar nchi hiyo ilitenga eneo maalum na kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya makazi kwa wale walioenda kutazama mechi za kombe la Dunia, eneo hilo pia lilikuwa na kiwanja cha mpira, eneo hilo ni Al-Thumama maarufu kama Al-Thumama complex katika mji wa Doha.

Mtoto na simulizi kupitia picha

Eneo hilo sasa limegeuzwa makazi ya dharura kwa zaidi ya wakimbizi 1,700 wa Kipalestina ambao waliondolewa nchini mwao wakati wa vita Kali kati ya majeshi ya Israel na wanamgambo wa Hamas vita ambayo imesitishwa hivi sasa. Wakimbizi hao wa kipalestina wakiwa katika eneo la Al-Thumama wanapatiwa matibabu ya kawaida, ya viungo na usaidizi wa kijamii.

Rais wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amefika katika eneo hilo ili kuwajulia hali.

Kwanza alikutana na watoto, video inamuonesha akizungumza na mtoto wa kiume ambaye ameandika kitabu kwa njia ya picha na ndoto yake ni kitafsiriwe kutoka kiarabu kwenda lugha mbalimbali. toto huyo akatia saini nakala ya kitabu chake na kumpa Rais wa Baraza Kuu.

Rais wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock (kati) akizungumza na mtoto wa kike kwenye makaziya Al -Thumana huko Doha, Qatar yanayojhifadhi wakimbizi wa kipalestina walioondolewa Gaza ili kupatiwa matibabu eneo hili.

UN News/Abdelmonem Makki

Rais wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock (kati) akizungumza na mtoto wa kike kwenye makaziya Al -Thumana huko Doha, Qatar yanayojhifadhi wakimbizi wa kipalestina walioondolewa Gaza ili kupatiwa matibabu eneo hili.

Watoto licha ya majeraha bado wana matumaini

Kisha, Rais Baerbock anaonekana akizungumza na familia nyingine, pembeni mtoto mmoja mwenye umri kama wa miaka mwili hivi mkono wake wa kulia unaonekana umekatwa chini kidogo ya bega. Mtoto huyo anarukaruka kwenye kochi huku wanafamilia yake wakizungumza na mgeni.

Anatoka akitembea kwenda eneo jingine lakini ndani ya eneo hilo hilo la Al-Thumama kwenye chuo cha ufundi stadi na kujionea namna wanawake wanavyojishughulisha na kazi za mikono ikiwemo ufumaji kwa kutumia mashine za kisasa za mkono. 

Akitoka huko akiwa na wanawake kadhaa akawa anaelekea eneo lenye hospitali … njiani akakutana na mwanamke akiwa kwenye kiti mwendo, wakasimama na mwanamke huyo akawapa vitafunywa wakala na kufurahia huku Rais wa Baraza Kuu akisifu kwa utamu wa vitafunio hivyo.

Rais wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock akizungumza na mwanamke mwenye kwenye makaziya Al -Thumana huko Doha, Qatar yanayojhifadhi wakimbizi wa kipalestina walioondolewa Gaza ili kupatiwa matibabu eneo hili.

UN News/Vibhu Mishra

Rais wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock akizungumza na mwanamke mwenye kwenye makaziya Al -Thumana huko Doha, Qatar yanayojhifadhi wakimbizi wa kipalestina walioondolewa Gaza ili kupatiwa matibabu eneo hili.

Baada ya hapo safari ya kwenda hospitali ikaendelea, na huko akakutana na madaktari na kujionea mashine mbalimbali za kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi wa kipalestina.

Ziara hiyo aliyoianza tangu mchana kweupe alihitimisha giza likiwa limeshatanda nje na akatoa ujumbe kwa dunia kile alichojionea.

Amesema, “nimeona yale hawa watoto walipitia, nyuso zao ziliungua kwa moto, wamepoteza mikono, wazazi, familia nzima, lakini bado wanaonesha ujasiri na wanamatumaini na maisha yao ya baadae, wakijaribu kurejea shuleni na hii inaweka mkazo wa jukumu letu ni lipi kama jumuiya ya kimataifa. Tunapaswa kukomesha kabisa mgogoro huu uliodumu kwa muongo mmoja, mzozo wa muda mrefu na kwamba amani ya kudumu haita hakikishwa kwa kupitia vita, ugaidi wala kukalia eneo kimabavu bali kwa makubaliano ya amani ya kuwa na mataifa mawili yanayojitegemea, kupelekea kwa taifa huru la Kipalestina ambapo kizazi kijacho kinaweza kuishi kwa heshima pia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *