Sudan imekariri wito wake kwa jamii ya kimataifa ikitaka kufanyika juhudi za kuzuia mtiririko wa silaha kwa wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) na kulitaja kundi hilo kuwa “taasisi ya kigaidi.”

Wito huu ulitolewa jana kwenye ubalozi wa Sudan mjini Addis Ababa Ethiopia na Balozi Al Zain Ibahim Hussein ambaye ni Mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Afrika. 

Balozi Hussein ameituhumu jamii ya kikanda na kimataifa kwa kuwawezesha wanamgambo wa RSF kutenda jinai katika mji wa El Fasher makao makuu ya jimbo la Darfur kaskazini na katika miji na vijiji vingine. 

Wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu waliuteka mji wa El Fasher na kufanya mauaji ya umati dhidi ya raia. Ripoti hii imetolewa na taasisi za ndani ya Sudan na za kimataifa. 

Mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Afrika (AU) ametaka kukomeshwa ukiukaji wa haki za binadamu na utumiaji mabavu kwa kusitisha ufadhili wa kifedha na silaha kwa wanamgambo w RSF. Balozi Al Zaib Ibrahim Hussein pia ameitaka jamii ya kimataifa kukiarifisha kikosi cha RSF kama taasisi ya kigaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *