Aidha, katika taarifa yake, EWURA imewataka wafanyabiashara wote wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa rejareja na jumla kuuza mafuta kwa bei zilizotangazwa na mamlaka hiyo na atakayekiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuchuliwa dhidi yake.

Pia, imevitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta ya petroli katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika ili pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja waweze kununua bidhaa hizo katika vituo vinavyouza kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Kwa mujibu wa EWURA, kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja ni kosa na adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *