Uchaguzi wa spika wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, unatarajiwa kufanyika Alhamisi, wiki ijayo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tarehe hii imetajwa wakati huu, muungano wa kisiasa wa Sacred Union wake rais Felix Thisekedi, ukimteua mbunge, Aimé Boji kuwa mgombea wake kwenye nafasi hiyo kumrithi Vital Kamerhe aliyejiuzulu.
Kwa mujibu wa taratibu za bunge, kuhusu uchaguzi huo, wagombea wanaotafuta nafasi hiyo, majina yao yatawasilishwa siku tatu kabla ya upigaji kura.

Kuanzia siku ya Jumamosi, Kamati maalum iliyoundwa na bunge, itaanza vikao rasmi vya kupigia majina ya wagombea na iwapo wamekidhi masharti ya kuwania Uspika.
Kabla ya wabunge kupiga kura, wagombea watapata fursa ya kufanya kampeni Novemba tarehe 11 na 12, kabla ya zoezi hilo kufanyika, na mshindi ataapishwa baada ya uchaguzi kumalizika.