
Duru za Umoja wa Mataifa zimeripoti kuwa askari usalama vya Cameroon wameuwa raia 48 katika maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena Rais Paul Biya, mtawala mzee zaidi duniani.
Duru hizo zimearifu kuwa aghalabu ya wahanga wameuliwa na silaha moto licha ya raia kadhaa kupoteza maisha kutokana na majeraha waliyopata yaliyosababishwa na vipigo vya marungu na fimbo.
Serikali ya Biya mwenye umri wa miaka 92 hadi sasa haijatangaza idadi rasmi ya waandamanaji waliouawa na askari usalama.
Wiki iliyopita Biya alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa Rais baada ya kuibuka na ushindi wa asilimia 53.66% ya kura dhidi ya mpinzani wake kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma Bakary aliyepata asilimia 35.19 ya kura zilizopigwa. Bakary ni msemaji wa zamani wa serikali ambaye alijiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mwezi Juni mwaka huu.
Issa Tchiroma Bakary alijitangaza kuwa mshindi muda mfupi baada ya uchaguzi wa Oktoba 12, na maandamano yalizuka katika maeneo mbalimbali ya Cameroon kwa kuwa matokeo ya awali yalionyesha kuongoza Paul Biya ambaye amekuwa madarakani tangu 1982.
Shirika la kiraia linalojulikana kwa jina la Stand Up for Cameroon lilisema wiki iliyopita kwamba takriban watu 23 wameuawa katika makabialiano kati ya askari usalama na waandamanaji.
Rais mteule Paup Biya anatazamiwa kuapisha kesho Alhamisi kuingoza Cameroon kwa muhula wa nane.