Kulingana na taarifa za Umoja Mataifa, mashambulizi hayo yalifanyika mji wa El- Obeid dhidi ya watu waliokuwa matangani. Katika taarifa hiyo, shirika ya Umoja Mataifa la OCHA limeelezea kuwa idadi nyingine ya watu isiyojulikana walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Mashambilizi hayo yametokea wakati watu wakiendelea kukimbia kutoka eneo la El- Fasher lililotekwa na wapiganaji wanamgambo wa  RSF.

Watu hao wamesimulia kuhusu maovu makubwa yanayofanywa dhidi ya binadamu na wapiganaji hao ikiwemo ubakaji. Mama mwenye watoto wanne kwa jina bandia la  Amira ambaye kwa sasa anaishi katika kibanda cha muda eneo la Tawila umbali wa kilomita 70 kutoka El Fasher, amesimulia jinsi magenge ya wabakaji yanavyoendesha maovu hayo waziwazi.

Aliongezea kuwa watu ambao hawangeweza kuwalipa wavamizi hao wasiwadhuru mabinti, dada na wake zao, waliishia kuwaona jamaa zao wakibakwa hadharani. Hata hivyo, kuna taarifa kwamba pande zote mbili katika mzozo huo zinahusika katika kutenda maovu hayo.

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) wametoa taarifa kuwa wanawatunza  zaidi ya waathirika wa ubakaji 300.

Waathirika hao walitokea kambi ya Zamzam ambapo kufuatia mashambulizi ya RSF, zaidi ya watu 380,000 waliokuwa wakiishi hapo walikimbia.

Misaada zaidi inahitajika Sudan

Mashirika ya kibinadamu yamesema kuwa watu waliokimbilia usalama wao wanahitaji chakula,maji, dawa, makazi na pia kuwapa maliwazo kuondokana na kuteseka kimawazo na unyanyapaa wakiyakumbuka yale waliopitia.

Farhan Haq ambaye ni naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja Mataifa amefahamisha licha ya mazingira magumu lakini bado huduma za kibadamu zinatolewa.

Kurejea kwa Riek Machar Sudan Kusini

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

“licha ya mazingira hatari zaidi ya kuendesha operesheni za kibindamu, washirika wetu wanaendelea kutoa huduma na misaada kule wanakoweza kufika. Kutokana na kiwango cha juu na mahitaji ikilinganishwa na kushuka kwa ufadhili, tunatoa mwito kwa wahisani kuzidisha misaada ya kibinadamu kwa dharura.”

Kuteka mji wa El-Fasher kumewezesha RSF kuwa na udhibiti wa miji yote mitano mikuu katika eneo la Darfur. Hali hii inalewa wasiwasi kwamba sasa nchi hiyo yaweza kugawanywa mara mbili yaani upande mmoja ukidhibitiwa na RSF na mwingine na jeshi la serikali.

Baada ya kuteka El- Fasher ambayo ndiyo ilikuwa ngome kuu ya majeshi ya serikali, wanamgambo wa RSF wanashukiwa kupanga kuvamia Kordofan  

Jamii ya kimataifa imeikosoa mara kadhaa Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kutoa silaha kwa RSF. Lakini nchi hiyo imekanusha   madai hayo mara kadhaa. Kulingana na wachunguzi,jeshi la Sudan linaungwa mkono na kupata misaada kutoka nchi za Misri, Saudia, Uturuki na Iran.

Mashirika ya kibinadamu yamesema kuwa watu waliokimbilia usalama wao wanahitaji chakula,maji, dawa, makazi na pia kuwapa maliwazo kuondokana na kuteseka kimawazo na unyanyapaa wakiyakumbuka yale waliopitia. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *