
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema Brenda Rupia akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar es Salaam, amesema mioyo ya Watanzania inavuja damu hivi sasa, kwasababu hilo ni jambo jipya kwao.
Lori za jeshi zaripotiwa kubeba maiti za waandamanaji
Ofisa mwingine wa Chadema, Deogratius Munishi, amesema alipokea ujumbe jana kutoka kwa raia karibu na mji wa Arusha ambao waliripoti kuona lori mbili za jeshi zikitoka kwenye eneo la vyumba vya kuhifadhia maiti zikiwa zimejazwa miili ya waliouawa.
”Siku chache zilizopita tulisikia taarifa kuwa polisi wanakwenda katika hospitali mbalimbali kuchukua maiti za waliouawa wakati wa maandamano na tunasikia baadhi yao wanazikwa kwenye makaburi ya pamoja, kwa hiyo, haya ndiyo mambo ambayo tunataka vyombo vya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa vije kuyathibitisha.”Mashirika ya haki na wadau mbali mbali wamelaani mauaji hayo nchini Tanzania.