
Nchini Sudan, shambulio katika hafla ya mazishi katika mji wa El-Obeid kwenye eneo la Kordofan limewaua watu 40, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, huku wanajeshi wakionekana kuwa tayari kufanya mashambulio.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika la Umoja wa Mataifa la kibinadamu halikubainisha ni lini shambulizi hilo lilifanyika au nani alihusika katika shambulizi hilo, lakini limesema kuwa hali katika eneo la Kordofan inaendelea kuwa mbaya zaidi.
Vita nchini Sudan ambavyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao vimeenea katika maeneo mapya katika siku za hivi karibuni na hivyo kuzua hofu ya kutokea maafa makubwa zaidi ya kibinadamu.
Kikosi cha RSF, kilikuwa kinajiandaa kufanya mashambulizi huko Kordofan baada ya kuteka eneo la El-Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi katika eneo kubwa la magharibi la Darfur.
Raia wamelazimika kulikimbia eneo la El-Fasher kwa kile wamekielezea ni unyanyasaji wa kutisha, ikiwa ni pamoja na ubakaji, mikononi mwa RSF.
Madaktari Wasio na Mipaka MSF wamesema zaidi ya watu waathirika 300 wa unyanyasaji wa kijinsia wametafuta huduma kutoka kwa madaktari wake katika eneo la Tawila baada ya shambulio la awali la RSF kwenye kambi ya karibu ya Zamzam.
RSF sasa inatawala mji wa Darfur na sehemu za kusini, wakati jeshi linashikilia mikoa ya kaskazini, mashariki na kati kando ya Nile na Bahari Nyekundu.
Wakati huo huo, jeshi la Sudan limepata msaada kutoka taifa la Misri, Saudi Arabia, Uturuki na Iran.