Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kiutu, OCHA, haikubainisha ni lini shambulizi hilo lilifanyika au nani aliyehusika, lakini imesema hali katika eneo la Kordofan inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Kundi la RSF ambalo limekuwa vitani na jeshi la serikali tangu mwaka 2023, linapanga kufanya mashambulizi Kordofan baada ya kuiteka El-Fasher, ngome ya mwisho ya jeshi katika eneo kubwa la Darfur Magharibi.

OCHA yazitaka pande zinazozozana Sudan kuwalinda raia

Kwa mara nyingine tena, OCHA imetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama na kwa pande zote husika kuwalinda raia na kuheshimu sheria ya kimatifa ya kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *