Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amekosoa tuzo ya Nobel ya Amani ya mwaka 2025, na kusema tuzo hiyo imepoteza uhalali wake kutokana na kupewa kwa Maria Corina Machado, ambaye amemsifu Benjamin Netanyahu licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, Araghchi amesema kuwa tuzo ya Nobel ya Amani ya Nobel “imeshakuwa chombo cha kisiasa dhidi ya serikali zisizo za Magharibi.” Ameongeza kuwa tuzo hiyo imepoteza heshima yake kwa sababu “imekuwa ikitumika mara kwa mara kushambulia serikali zinazochukuliwa kuwa wapinzani wa maslahi ya Magharibi.”

Araghchi amebaini kuwa kupewa tuzo hiyo kwa “mtu anayechochea vita dhidi ya nchi yake mwenyewe huku akiwatukuza wanaotekeleza mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita Palestina” kunathibitisha zaidi mtazamo huo.

Maria Corina Machado, mwanasiasa wa upinzani kutoka Venezuela na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2025, aMEjigamba kuhusu mazungumzo ya simu na Netanyahu, ambapo ametoa msaada wake kwa kampeni ya mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza. Machado amezitaja  harakati za kupigania ukombozi za Hamas, Hizbulla, na Ansarullah kuwa eti ni “magaidi.”

Machado pia amewahi kuunga mkono mpango wa  Rais wa Marekani Donald Trump wa kuingilia kijeshi nchini Venezuela.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imeshatoa waranti wa kukamatwa Netanyahu kutokana na uhalifu wa kivita na dhidi ya ubinadamu huko Gaza. Kwa mujibu wa sheria za ICC, mataifa yote 125 wanachama wa mahakama hiyo yanawajibika kumkamata Netanyahu endapo ataingia katika maeneo yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *