
Zohran Mamdani amewashinda gavana wa zamani Andrew Cuomo na mgombea wa Republican Curtis Sliwa.
Mamdani, mzaliwa wa Uganda mwenye asili ya Kihindi, amekuwa Meya wa kwanza Mwislamu na mwenye asili ya Asia Kusini katika historia ya mji huo.
Kampeni yake ilijikita katika masuala ya gharama za maisha, akihaidi kusimamisha ongezeko la kodi ya nyumba, kutoa usafiri wa umma bure, na kuongeza kodi kwa matajiri.