Mashambulizi hayo yameanza muda mfupi baada ya jeshi la Israel kutoa tahadhari kwa wakaazi kwenye eneo la mpakani la Tayber, maeneo ya Tayr Deba na Aita al Jabal. Jeshi la Israel limesema makaazi lililoyalenga yamekuwa yakitumiwa na wapiganaji wa Hezbollah.

Hezbollah yashutumiwa kwa kujijenga upya kijeshi

Israel, inalishutumu kundi hilo kwa kujijengea upya uwezo wake wa kijeshi,  mwaka mmoja baada yakuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya  kusitisha vita vilivyodumu kwa miezi kadhaa.

Mashambulizi dhidi ya Hezbollah yamefanywa muda mfupi baada ya wanamgambo hao kuionya serikali ya Lebanon kuwa haipaswi kushinikizwa kuingia kwenye mazungumzo mapya na Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *