Madrid, Hispania. Klabu ya Real Madrid imeweka wazi msimamo wake kuhusu hatma ya kiungo mshambuliaji kutoka Brazil, Vinícius Jr.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Defensa Central, licha ya kuwepo kwa sintofahamu kuhusu mkataba mpya wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, mabingwa hao wa Hispania hawana mpango wowote wa kumuuza.

Ripoti hiyo inadai kuwa, rais wa Real Madrid, Florentino Pérez, amezungumzia suala hilo katika kikao cha bodi, na ujumbe wake ulikuwa wazi na wa moja kwa moja kwa wajumbe wengine.

VINI Jr Pict

Pérez amesisitiza kuwa klabu hiyo haizingatii kumuuza Vinícius, licha ya uvumi unaomhusisha kuhusu klabu za Saudi Arabia, zinazotajwa kumwania katika kipindi hiki.

Badala ya kufikiria uhamisho, mpango wa Real Madrid ni kufungua tena mazungumzo ya kuongeza mkataba mara msimu huu utakapoisha.

Uvumi unaodai kuwa Vini Jr anaweza kuondoka karibuni unatajwa kuwa hauna ukweli wowote.

Vinícius, ambaye bado ana mkataba unaodumu hadi mwaka 2027, hajawahi kuficha mapenzi yake kwa Real Madrid. Malengo yake yamekuwa kuendelea kuchezea klabu hiyo ya Santiago Bernabéu na kupigania mataji makubwa ya Ulaya.

Akiwa na umri wa miaka 25, mshambuliaji huyo bado ana miaka yake bora zaidi ya soka. Ingawa kwa sasa hakujafikiwa makubaliano mapya kutokana na tofauti za kifedha, hali ndani ya klabu inajaa matumaini kwamba makubaliano hayo yatafikiwa hivi karibuni ili kuthibitisha mustakabali wake wa muda mrefu.

VINI 02

Kwa sasa, Vinícius na washauri wake wanaendelea kuwa watulivu, wakifahamu kuwa mkataba wa sasa unamlinda, huku wakitambua pia muda unawapa nguvu zaidi katika mazungumzo hayo.

Hata hivyo, Real Madrid inapendelea kuanza mazungumzo hayo mapema ili kumaliza uvumi unaoendelea na kuepuka hali ya hatari, ambapo msimu wa kiangazi wa 2026 ukikaribia, huku nyota wao mkubwa akiwa na mwaka mmoja pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *