Marekani imetishia kupinga kurejeshwa kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Abyei, eneo lenye mzozo kati ya Sudan iliyokumbwa na vita na Sudan Kusini, mpaka pande zote mbili zitakapoyakubali makubaliano ya amani ya 2011.

Katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana Jumatano, balozi wa Marekani katika umoja huo Mike Waltz alianisha masharti ya Marekani ya kurefusha kwa mamlaka yakikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Abyei (UNISFA), ambayo yanafika mwisho Novemba 15.

Waltz aliliambia Baraza la Usalama kwamba Sudan na Sudan Kusini lazima sasa zitekeleze ahadi zao kwa makubaliano ya amani ya 2011 na mamlaka ya UNISFA ili kupata uungwaji mkono wa Marekani kwa urerushaji wa mamlaka ya kikosi hicho.

Waltz alisema pia nchi hizo jirani zinahitaji kuhakikisha kwamba Abyei ni eneo lisilo na wanajeshi, kuanzisha mipango ya muda ya kiutawala na usalama kama vile kikosi cha pamoja cha polisi cha Abyei, na kubaini hadhi ya mwisho ya eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *