Viongozi wa Sudan wametupilia mbali pendekezo la kusitisha vita lililotolewa na Marekani, Waziri wa Ulinzi wa Sudan alitangaza kwenye televisheni siku ya Jumanne, Novemba 4. Tangu Septemba, Massad Boulos, mjumbe wa Marekani kwa Afrika, amekuwa akifanya majadiliano na washirika wa kikanda ili kukamilisha makubaliano haya. Jijini Nairobi, Kenya, balozi wa Sudan aliweka wazi msimamo wake siku ya Jumatano, Novemba 5.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix

Kwa mamlaka za Sudan, hakuna suala la kujadiliana na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Jenerali Hemedti. Wanawachukulia kama wanamgambo wanaojihusisha na mauaji ya kimbari ambao wanapaswa kulaaniwa na jumuiya ya kimataifa. Kwa hivyo mamlaka huko Port Sudan inakataa pendekezo la Marekani. “Tumewasilisha pendekezo lapingamizi kwa serikali ya Marekani. Kundi la wanamgambo wa RSF linapaswa kuvunjwa. Linapaswa kutangazwa kama kundi la kigaidi.” “Na viongozi wake lazima wafikishwe mbele ya sheria. Hilo ndilo suluhisho pekee lililopo,” anasisitiza Mohamed Osman Akasha, balozi wa Sudan jijini Nairobi.

Balozi alitumia fursa hiyo kuonyesha unafiki wa jumuiya ya kimataifa, ambayo, kwa maoni yake, bado inakataa kukubali jukumu la Falme za Kiarabu katika mzozo huo. Mnamo mwezi Januari 2024, jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa liliandika usaidizi wao wa vifaa na kifedha kwa kundi la wanamgambo wa RSF.

Khartoum inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukuwa hatua

“Wakati huo huo, mfadhili mkuu wa RSF anaendelea kuajiri mamluki wa kigeni, na kubadilisha wanamgambo hawa kuwa mtandao wa kimataifa wa wafadhili wenye silaha na viongozi wa kivita.” “Ikiwa jumuiya ya kimataifa inataka kweli kuonyesha kujitolea kwake kwa amani na ubinadamu nchini Sudan, lazima ichukue hatua madhubuti ili kuzuia mtiririko wa silaha, mamluki, na ufadhili kwa Vikosi vya RSF,” ameongeza Mohamed Osman Akasha.

Siku ya Jumanne, msemaji wa Ikulu ya White House alisisitiza kwamba Marekani inaendelea “kushiriki kikamilifu” katika kutafuta suluhisho la mgogoro nchini Sudan, pamoja na washirika wake: Misri, Saudi Arabia, na Falme za Kiarabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *