Baadhi ya viongozi wa Dunia wamewasili nchini Brazil na kutembelea msitu wa Amazon ikiwa ni katika juhudi za kujaribu kuonesha dunia kuwa suala la mabadiliko ya tabia nchi bado linasalia kipaumbele chao licha kutotimizwa kwa ahadi na Marekani kuonesha ukaidi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kuanzia leo na kesho Wakuu wa nchi na Serikali zaidi ya 50 wanatarajiwa kuhudhiria kongamano la mazingira kwenye mji wa Belem nchini Brazil, ikiwa ni kikao cha awali kuelekea kilele cha mkutano wa makadiliano kuhusu tabia nchi utakaong’oa nanga tarehe 10 hadi 22 ya mwezi huu.

Wakati huu karibu kila nchi duniani inatarajiwa kutuma angalau wawakilishi kadhaa, Marekani peke yake ndio haitakuwa na uwakilishi, ambapo rais Donald Trump ameuita mkutano huu wa kisayansi wa COP30 kama ‘wizi’.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akihudhuria mikutano kabla ya mkutano wa COP30, mjini Belem
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akihudhuria mikutano kabla ya mkutano wa COP30, mjini Belem REUTERS – Anderson Coelho

Waziri mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron watahudhuria mkutano wa Belem, huku wachafuzi wengine wakubwa wa mazingira kama Uchina na India, wenyewe wakituma manaibu wao.

Licha ya wanaharakati kuonesha imani ndogo kwa viongozi watakaokutana kupata muafaka kuhusu kukabiliana na athari za tabia nchi, lakini bado wanaamini nafasi iko kwa wajumbe kutoka na maazimio yatakayoridhiwa na kila nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *