Kazakhstan imesema inatarajia kujiunga na Makubaliano ya Abraham kati ya Israel na mataifa mengi ya Kiislamu, katika hatua kubwa ya ishara inayolenga kuongeza msukumo wa Rais wa Marekani Donald Trump wa amani ya Mashariki ya Kati.

Jamhuri hiyo ya Asia ya Kati imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Israel kwa miongo kadhaa, tofauti na mataifa manne ya Kiarabu yaliyorejesha uhusiano na Israel chini ya makubaliano ya awali yaliyosainiwa katika muhula wa kwanza wa Trump.

Tangazo kwamba Kazakhstan itajiunga na makubaliano ya Abraham lilitarajiwa kuja wakati Trump atakapomkaribisha Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev na viongozi wa jamhuri nyingine nne za Asia ya Kati katika Ikulu ya White House jana.

Kazkahstan itakuwa nchi ya kwanza kujiunga tangu Makubaliano ya awali ya Abraham mwaka wa 2020, wakati Jumuiya ya Falme za Kiarabu, Bahrain na Morocco ziliporejesha mahusiano na Israeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *