
Wawili hao walitoweka mwezi Oktoba baada ya kusafiri nchini Uganda kumuunga mkono kiongozi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine, ambaye anagombea urais dhidi ya rais wa muda mrefu Yoweri Museveni katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Katika taarifa ya pamoja kwenye mtandao wa X iliyochapishwa na mkuu wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya, LSK, Faith Odhiambo, mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty Kenya, Vocal Africa na LSK, yamesema yanapongeza hatua ya kuachiwa huru kwa wanaharakati hao Oyoo na Njagi jana usiku huko Busia baada ya siku 38 za kutoweka kwao.
Hata hivyo taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi lakini imesema inafanya mipango ya kuwasafirisha wawili hao hadi Nairobi.