
Kulingana na taarifa ya jeshi na Umoja wa Mataifa, wanajeshi wawili na sungusungu wawili waliuawa katika shambulio hilo.
ISWAP ilijitenga na kundi la kigaidi la Boko Haram 2016 na limejielekeza katika kushambulia jeshi la Nigerian.
Mashambulizi ya kigaidi yamewaua watu zaidi ya 40,000 na kufanya watu karibu milioni mbili kaskazini mashariki mwa kuondolewa katika makazi yao tangu 2009, na yameendelea hadi katika nchi jirani ya Niger, Chad na Cameroon.
Uba ni afisa wa pili mwandamizi wa jeshi kuuawa na magaidi katika kipindi cha miaka minne, baada ya Jenerali Dzarma Zirkusu, aliyeuawa Novemba 2021.