LIGI ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (NBL) inayoendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa Chinangali mkoani Dodoma imelamba udhamini wa Sh317,025,900 kutoka kampuni ya BetPawa.

Kupitia mkataba huu mpya, kampuni hiyo pia imetenga Sh13 milioni kwa ajili ya tuzo za timu na wachezaji, zikiwamo tuzo za Mchezaji Bora (MVP), Mfungaji Bora na nyinginezo zinazolenga kutambua nyota wa msimu.

Udhamini huu mpya unaendeleza mpango wa Locker Room Bonus (LRB), mfumo wa kipekee wa motisha unaotoa  Sh140,000 papo hapo kwa kila mchezaji baada ya kila ushindi katika mechi, kuhakikisha wachezaji wanahisi thamani ya mchango wao mara moja baada ya mchezo.

Mfumo huo umepata sifa kubwa Afrika kwa kubadilisha namna wachezaji wanavyojihusisha na mashindano, kwa kuwazawadia kwa jitihada zao na kuongeza kiwango cha ushindani.

Athari zake zilionekana wazi Tanzania wakati wa michezo ya mtoano msimu uliopita, ambapo uliwaongezea nguvu na ari wachezaji na timu.

Akizungumzia kuhusu kuendelezwa kwa udhamini huo, Borah Ndanyungu, Mkuu wa Masoko ya Ndani na CSR wa kampuni hiyo amesema: “Tunajivunia kuendelea kuunga mkono mpira wa kikapu hapa Tanzania. Locker Room Bonus imeonekana kuwa chachu kubwa ya motisha kwa wachezaji, na udhamini huu unaonyesha imani yetu ya muda mrefu katika kukuza mchezo huu. Tunazingatia na kuthamini juhudi, kuhamasisha vipaji na kuhakikisha kila ushindi una maana kwa wale wanaoufanyia kazi.”

Viongozi wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF), wameukaribisha udhamini huo, wakibainisha kuwa kampuni  hiyo inaendelea kuweka viwango vipya katika ustawi wa wachezaji, motisha na ushirikishaji wa mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *