Kwa mjibu wa ofisi yake, Macron atapigania ajenda ya ushirikiano katika masuala ya uchumi na biashara inayolenga kufikia uwiano unaohakikisha “ukuaji endelevu, imara na wenye manufaa kwa wote.” Ufaransa inalenga kuvutia uwekezaji zaidi kutoka kwa kampuni za China na kurahisisha upatikanaji wa masoko kwa bidhaa za Ufaransa. Wakati wa ziara hiyo, maafisa kutoka mataifa yote mawili wanatarajiwa kusaini makubaliano kadhaa katika sekta za nishati, chakula na anga. Ufaransa itakuwa mwenyeji wa mkutano nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 mwaka 2026 unaohusisha uchumi mkubwa zaidi duniani, huku China ikitarajiwa kuongoza jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki (APEC) lenye wanachama 21, wakiwemo Marekani, Korea Kusini, Japan, Australia na Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *