Kamanda wa manuva ya kupambana na ugaidi ya “Sahand 2025” ameuelezea ujumbe wa mazoezi hayo ya kijeshi kuwa ni juhudi za pande zote za kupambana na ugaidi, akisema: “Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na vya nchi zilizoshiriki vimefanikiwa kutekeleza sinario za manuva hayo”.

Akizungumza katika mahojiano mwishoni mwa mazoezi ya kijeshi ya kupambana na ugaidi ya Sahand 2025, Brigedia Jenerali Vali Mani, kamanda wa manuva ya kupambana na ugaidi ya Sahand 2025 na naibu kamanda wa Operesheni za Vikosi vya Nchi Kavu vya IRGC, amesema: “manuva haya yalibuniwa kwa kutumia dhana kwamba magaidi wana uwezo mzuri, na kwa mantiki tuliyokuwa nayo na kulingana na hali ya mazoezi, hatukuruhusu magaidi kukaribia hata ukuta wa mpaka.”

Brigedia Jenerali Mani ameongezea kwa kusema: “tuna nyenzo nzuri na timu zetu maalumu zilifanya vizuri sana katika mazoezi hayo; utendaji na ubora wa ndege zisizo na rubani na ndege ndogo ndogo ulikuwa nzuri sana, na operesheni za hujuma na za mashambulizi zilibuniwa vizuri kulingana na hali ya mazoezi.”

Kamanda wa mazoezi ya kupambana na ugaidi ya Sahand 2025 amesema: “timu za mashambulizi za Vikosi vya Nchi Kavu vya IRGC ziliangamiza pia timu za kigaidi zilizokuwa zinajaribu kuingia nchini mwetu kutokea nchi nyingine, ndani kabisa ya ardhi ya nchi hiyo”.

Halikadhalika ameeleza kwamba: “katika mwendelezo wa manuva, helikopta zetu za mashambulizi ziliteketeza mabaki ya magaidi kulingana na hali ya mazoezi; zoezi hilo pia lilifanywa kwa ushirikiano na nchi wanachama za Shanghai, na sehemu nyingine ya mazoezi hayo iliendeshwa kwa mafanikio na Kikosi cha Nchi Kavuu cha IRGC”…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *