Jumuiya ya Kiuchumi Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) imetangaza hali ya hatari, huku eneo hilo likiendelea kukumbwa na hitilafu za kisiasa.
“Matukio ya hivi karibuni yanaonesha mustakabali halisi wa eneo letu katika siku zijazo, na hivyo kuwepo na haja ya kuwekeza kwenye usalama wa eneo letu,” alisema rais wa jumuiya hiyo Oumar Touray katika mkutano wa ngazi ya mawaziri uliofanyika Abuja, nchini Nigeria.
Tangazo la ECOWAS linakuja siku chache baada ya jaribio la mapinduzi kushindikana nchini Benin.