Dar es Salaam. Mwaka 2025 unaenda ukingoni kabla ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2026. Ni mwaka ambao yametokea mengi kwenye burudani ikiwamo mabadiliko makubwa kwa wasanii wa Bongo Fleva, vipaji vyenye ubunifu na uthubutu vikiibuka na kuwa gumzo kwa mashabiki wa kazi zao.

Wapo chipukizi katika Bongo Fleva, Hip Hop hadi Singeli ambao walithibitisha wana njaa ya mafanikio na katika vyombo mbalimbali vya habari, ikiwamo redio, mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya kidijitali wakishirikiana na wasanii wenye majina makubwa, wamepenya kwenye mioyo ya mashabiki na kuutikisa mwaka huu.

Katika kuibuka kwao, wapo waliopitia kwa wasanii wakubwa, walioonyesha ubunifu wao katika mitandao kama Tik Tok na wengine kimya kimya hadi kukubalika kutokana na kuleta ladha mpya, kukuza soko la muziki, kuongeza ushindani na hapa Mwananchi linakuchambulia baadhi ya chipukizi hao ambao walifanya vizuri mwaka huu.

1.Dogo Paten

Milango yake kisanii ilifunguliwa na Zuchu aliyemposti baaada ya mwanadada huyo kupenda alichofanya Paten. Baada ya hapo, dogo huyo alitoa wimbo pamoja na Zuchu uitwao ‘Afande’ ambao kwa kiasi kikubwa ulimpasha.

Ngoma hiyo ilifanya vizuri mitaani, redioni, kwenye mitandao ya kijamii hususani YouTube na kufuatiliwa na watazamaji zaidi ya milioni tatu, ikifuatiwa na shoo mfululizo ikiwamo kuimba kwenye sherehe za watu maarufu kama Marioo.

Baada ya wimbo huo wa Afande, alitoa nyingine kali kama ‘Sikupendi’ na ‘Ungewezaje’ na zote zimefanya vizuri na kutajwa kama mmoja wa chipukizi watakaoleta mapinduzi makubwa kwenye Singeli.

2.Black Queen

Wakati muziki wa Hiphop ukionekana kupoa hasa kwa wanawake, mwanadada Black Queen akaibuka na kutingisha haswa.

Wasanii kama Rosa Ree na Chemical hawajatoa kibao chochote, huku Frida Amani ndiye rapa pekee aliyetoa ngoma kali iliyofanya vizuri ya ‘Wewe na Mimi’ akimshirikisha Jay Melody.

‘Single Mama’ na ‘Nakusubiri’ ni baadhi ya kazi zilizombeba ukichanganya na staili yake ya kuchana iliyowadatisha mashabiki wanaomfananisha na Rosa Ree na kumtabiria kuleta ushidani katika muziki huo.

Ngoma zake za ‘Wadaima’ na ‘Muongo’ zinazidi kumnyanyua hasa kutokana na kusikilizwa na zaidi ya watu laki tano katika mtandao wa YouTube.

Mwaka huu ameachia ngoma nyingi lakini hizo mbili zinapasua anga la muziki zikiingia pia kati ya nyimbo 20 bora kwa zinazosumbua, huku akitarajiwa kukutana na ushindani wa nyota wakubwa kama Alikiba, Harmonize na wengine wengi. Atatoboa? Tusubiri tuone.

Aliibuka mshindi wa pili kwenye mashindano ya kusaka vipaji vya Bongo Star Search (BSS), huku mshindi wa jumla akiibuka Moses Luka kutoka DRC Congo.

Katika mashindano yale, Saluh alikuwa mmoja ya vijana waliofanya vizuri kutokana na kipaji chake cha kuchanganya sauti na nyimbo mbalimbali kwa mtindo wa kipekee.

BSS ilikuwa kama platformu ya Saluh kutambulika kimuziki kwani baada ya ushindi huo, hakukawia na miezi michache baade akaachia ngoma nne, huku nyingine zikiwa ni ‘kava’ za wasanii wa zamani.

Hata hivyo, ngoma yake ya ‘Raha’ aliyoiachia miezi miwili iliyopita imefanya vizuri zaidi na kutazamwa sana YouTube na kuzidi kumnyanyua kisanii. 

5. Kondela

Alianzia mitandaoni akiwa na wasanii wengine kama Aslam na Yammi aliyewahi kusainiwa na Lebo ya African Princess inayosimamiwa na Nandy, kabla ya kuachana nayo.

Aliibuka na kibao chake cha ‘Day by Day’ na kuwabamba mashabiki wa muziki wa Kompa, huku wasanii wenzake Aslam akitoka kivyake na ngoma ya Tukutane Mwakani iliyofanya vizuri na Yammi akitamba na ngoma kama ‘Namchukia’, ‘Kukupenda’ na nyinginezo.

Kondela amekuja kitofauti na ngoma hiyo ambayo inaongoza kwa kufanyiwa chalenji nyingi kwenye mtandao wa Tik Tok na mashabiki kutoka nchi mbalimbali za nje hasa Haiti na Ufaransa.

6.Mama Amina

Msanii mwengine anayefanya vizuri kwenye muziki wa Singeli ni Mama Amina anayetamba na nyimbo kama ‘Tia Mguu’ aliyoshirikiana na Dj Pacheko na Mkadebe na ‘Nuna’ (Pacheko na Chinno Kidd).

Kwa mwaka huu ukitaja wasanii waliochipukia na kufanya vizuri ni pamoja na mwanadada huyo ambaye amefanya muziki uonekane kitu rahisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *