
Takriban watu 21 wamefariki dunia kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika mkoa wa Safi, ulioko kilomita 330 kusini mwa Rabat, nchini Morocco, mamlaka ya nchi hiyo imesema.
Mafuriko hayo pia yamejeruhi watu 32 siku ya Jumapili, na wengi wao wamepata matibabu na kutoka hospitalini, mamlaka imesema katika taarifa.