Mama wa mwandishi wa habari wa michezo wa Ufaransa Christophe Gleizes, aliyehukumiwa kifungo cha miaka saba jela mwanzoni mwa mmwezi Desemba nchini Algeria, ametuma ombi la msamaha kwa Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, kulingana na barua ya Desemba 10 na iliyoonekana na shirika la habari la AFP leo Jumatatu.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Ninawaomba kwa heshima mfikirie kumsamehe Christophe, ili apate tena uhuru wake na kuungana na familia yake,” ameandika Sylvie Godard katika barua hiyo, akisema kwamba alikuwa akiomba “nia njema” ya rais wa Algeria.

Mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 36 pia amewasilisha rufaa dhidi ya hukumu aliyopewaili kupata kesi mpya, mawakili wake walitangaza siku ya Jumapili.

Christophe Gleizes, anayefanya kazi na majarida ya Ufaransa ya So Foot na Society, alikamatwa Mei 28, 2024, nchini Algeria, ambapo alisafiri kuripoti kuhusu klabu ya mpira wa miguu iliyofanya vizuri zaidi nchini humo, Jeunesse Sportive de Kabylie (JSK), yenye makao yake Tizi-Ouzou, kilomita 100 mashariki mwa Algiers.

Mnamo Desemba 3, 2025, Mahakama ya Rufaa ya Tizi-Ouzou ilithibitisha kifungo chake cha miaka saba jela kwa “kuomba msamaha kwa ugaidi.” Vyombo vya sheria vya Algeria vinamtuhumu kwa kuwa na mawasiliano na watu binafsi waliohusishwa na MAK (Movement for the Self-Determination of Kabylia), kundi la wanaharakati wanaotaka kujitenga lililoainishwa kama kundi la kigaidi nchini Algeria.

“Uthibitisho wa kifungo cha miaka saba jela ulikuwa mshtuko mkubwa kwa Christophe, kama ilivyokuwa kwangu na familia yangu,” Bi. Godard ameandika katika barua yake kwa mkuu wa nchi wa Algeria, ambapo almesema ameiandika “kwa uzito na hisia kali.”

“Hukumu hii haieleweki kwetu kwa kuzingatia ukweli na historia ya mwanangu,” ameongeza. “Hakuna mahali popote katika maandishi yake yoyote ambapo utapata alama yoyote ya kitu chochote chenye uadui kwa Algeria na raia wake.”

Siku mbili baada ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliona hukumu iliyotolewa kwa Christophe Gleizes kuwa “iliyopitiliza” na “isiyo ya haki,” akisema azimio lake la kupata “matokeo mazuri.”

“Udhalimu mkubwa” Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Shirika la Waandishi wa Habari Bila Mipaka (RSF), ambalo huratibu kamati ya usaidizi ya Christophe Gleizes, liliunga mkono ombi hili la msamaha “ili kukomesha dhuluma kubwa.”

“Sasa tunatoa wito kwa mamlaka ya Algeria kufanya uamuzi pekee unaowezekana katika kesi hii: kumwachilia Christophe na kumruhusu kurudi kwa familia yake haraka iwezekanavyo,” anaelezea Thibaut Bruttin, mkurugenzi mkuu wa shirika hilo hicho, aliyenukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Bw. Gleizes kwa sasa ndiye mwandishi pekee wa habari wa Ufaransa anayezuiliwa nje ya nchi.

Hukumu yake ya kwanza mnamo mwezi Juni 2025 ilikuja wakati wa kilele cha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Algeria, uliogubika haswa na kujiondoa kwa mabalozi wote wawili na kufukuzwa kwa wanadiplomasia kwa njia ya pande zote mbili.

Lakini uhusiano wa pande mbili ulionekana kuimarika baada ya Algiers kutoa msamaha na kumwachilia huru mwandishi wa Ufaransa na Algeria Boualem Sansal mnamo Novemba 12.

Kulingana na wakili wake wa Ufaransa, Emmanuel Daoud, Christophe Gleizes ana chaguo, pamoja na kukata rufaa ya msamaha na kuwasilisha rufaa kwa Mahakama ya Juu, ya kuwasilisha ombi la kuachiliwa huru kwa Mahakama Kuu, ambalo linaweza kuambatana na “ombi la marekebisho ya hukumu yake.”

“Pia ni muhimu sana, kisaikolojia, kwa Christophe kupinga hatia yoyote kwa sababu, kama alivyoiambia Mahakama, alikuwa akifanya kazi yake tu na hakukiuka maadili ya uandishi wa habari kwa njia yoyote,” wakili huyo amesema, kama alivyonukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumatatu.

2025 AFP

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *