Nchini Nigeria, watoto zaidi ya mia moja waliotekwa nyara kutoka shule ya Kikatoliki katika Jimbo la Niger waliachiliwa wiki iliyopita. Hii ilikuwa faraja kubwa kwa familia zao, lakini furaha yao haikuwa kamili, kwani zaidi ya wanafunzi mia mbili bado wanashikiliwa mateka msituni na watekaji nyara wao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki kadhaa za kushikiliwa mateka, watoto walioachiliwa huru walirudi Jumatatu jioni, Desemba 8, katika Shule ya St. Mary’s, shule ileile ambapo walitekwa nyara, ili kuungana tena na wazazi wao. Kwa mama huyu, Blessing Jammeh anasema, “tulijawa na furaha kwa kuungana tena na watoto zetu lakini bado kuna watoto wengine wanaoshikiliwa mateka na hatujui hatima yao”, ameongeza.

“Nina furaha, lakini pia nalia. Watoto wangu wawili walitekwa nyara. Mmoja tu amerudi; mwingine bado hajapatikana. Mtoto aliyerudi ilibidi alazwe hospitalini.” “Katika msitu, hali ilikuwa mbaya: kuumwa na mbu, maji machafu—aliugua,” mama huyo anasimulia.

Mtoto wake mwingine bado anashikiliwa na watekaji nyara, kama vile zaidi ya wanafunzi mia mbili kutoka Shule ya St. Mary’s. Hadithi hii inarudia kile ambacho wazazi wengine wamesikia kutoka kwa watoto wao. Samuel Bala, kiongozi wa chama cha wazazi, anasimulia hili.

Mazingira mahumu ya kushikiliwa mateka

“Watoto waliorudi wanaelezea hali ngumu sana za kushikiliwa mateka. Walishikiliwa mahali pabaya: hawakuweza kunawa, na hata kula ilikuwa tatizo. Miongoni mwa watoto ambao bado wanashikiliwa, baadhi yao ni wadogo sana, wenye umri wa miaka mitano au sita hivi. Ndiyo maana wazazi wanaisihi mamlaka kuingilia kati ili kuwaokoa watoto ambao bado wako msituni,” anaelezea.

Mamlaka haijatoa maoni yoyote kuhusu mazungumzo yanayowezekana au malipo ya fidia. Shule ya St. Mary’s bado imefungwa. Hakuna tarehe ya kufunguliwa tena kwa shule hiyo ambayo imetangazwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *