
Klabu hiyo imethibitisha jeraha hilo siku moja baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mainz katika uwanja wa Allianz Arena Jumapili.
Kwa mchezo wa mwisho wa mwaka huu dhidi ya Heidenheim, kipa chipukizi Jonas Urbig, mwenye umri wa miaka 22, atachukua tena nafasi ya kulinda lango. Urbig tayari ameshiriki katika mechi nne za mashindano msimu huu na anaendelea kupata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika kikosi cha vinara wa Bundesliga.
Bayern Munich, chini ya kocha Vincent Kompany, wameendelea kutamba bila kupoteza katika mechi 14 za mwanzo na sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tisa kileleni mwa msimamo. Hata bila Neuer, Bayern wanatarajiwa kuendeleza kasi yao ya ushindi.
Majeraha yamuandama Neuer
Baada ya mapumziko mafupi ya katikati ya msimu, Bayern watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Red Bull Salzburg tarehe 6 Januari 2026, kabla ya kurejea rasmi katika Bundesliga kwa kuwakaribisha Wolfsburg tarehe 11 Januari. Hata hivyo, bado haijulikani ni lini Neuer atakuwa tayari kurejea uwanjani.
Kipa huyo wa zamani wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 39 amekuwa akikumbwa na majeraha madogo kwa miaka ya hivi karibuni na kwa sasa hana mkataba wa msimu ujao. Hali hii inazua maswali kuhusu mustakabali wake katika Bayern Munich na hatma ya uchezaji wake katika kiwango cha juu.
Kwa sasa, mashabiki wa Bayern wanabaki na matumaini kwamba kikosi chao kitaendelea kutamba bila nahodha wao, huku Jonas Urbig akipewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake na kuimarisha safu ya ulinzi wa mabingwa hao wa Bundesliga.