Baada ya kusubiri kwa siku tatu kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi, hatimaye zaidi ya Warundi 500 walioishi na kufanya kazi katika jiji la Uvira, mkoani Kivu Kusini, ambalo liko chini ya udhibiti wa AFC/M23, wameweza kurudi nchini mwao siku ya Jumapili, Desemba 14.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zaidi ya Warundi 500 walioishi na kufanya kazi katika jiji la Uvira, ambalo liko chini ya udhibiti wa AFC/M23 mnamo Desemba 10, wameweza kurudi nyumbani Jumapili, Desemba 14. Baada ya kupanga foleni kwa siku tatu kujaribu kuvuka mpaka na kujiunga na familia zao, wote walionekana wamechoka.

“Walinzi wa nyumba niliyokuwa nikifanya kazi walikimbia, na waajiri wangu waliniacha. Hatujui walikokwenda, kwa hivyo nilibaki hapa peke yangu,” mwanamke mmoja amesema, huku mwingine akisimulia kwamba “alifanya kazi katika kitongoji cha Nyamyanda cha Uvira,” kabla ya kuongeza: “Sikuwa mfanyabiashara pekee wa Burundi mjini; tulikuwa wengi tu katika hali hiyo. Wazazi wetu walio wasiwasi na maisha yetu. Lakini hatuwezi kusema tunakimbia: tunarudi nyumbani, tukisubiri kuona kama inawezekana kurudi.”

Ingawa ilijadiliwa kati ya AFC/M23 na Bujumbura, kurejea kwa Warundi hawa kunakuja huku kukiwa na mvutano kati ya kundi la waasi na mamlaka ya Burundi, ikishirikiana na FARDC, katika mapigano yanayoukumba mkoa wa Kivu Kusini.

Ingawa Wakongo kadhaa wanaotaka kurudi DRC bado wamekwama Burundi, AFC/M23 inapendekeza kwamba ugumu huu wa kuvuka kati ya nchi hizo mbili sio kosa lake: inadai kwamba mpaka uko wazi upande wa Kongo, lakini kwamba mpaka kwa upande wa Burundi umefungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *