#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na maarifa ili kuleta tija katika kuwatumikia wananchi.
Ametoa rai hiyo jijini Dodoma katika kikao kazi na watumishi wote wa Wakala.
“Mnafanya kazi nzuri, ndani ya miaka mitano kazi kubwa imefanyika lakini hatupaswi kubweteka, wananchi waishio maeneo ya vijijini wanatutegemea kwenye suala la Nishati, hatupaswi kuwaangusha,” alisisitiza Mhandisi Saidy.
Mhandisi Saidy alisema kuwa kila Kitengo na Idara ndani ya Wakala kina jukumu na wajibu wa kufanya ili kutimiza dhamira ya Serikali la kuwasambazia wananchi wake Nishati bora na aliwaasa watumishi wote kufanya kazi kwa kushirikiana bila kutazama Idara ama Kitengo anachotoka.
“Tufanye kazi, sisi ni timu moja, tuepuke kuwa chanzo cha migogoro, kama kuna jambo linakutatiza zungumza na watumishi wenzako, nenda kwa wahusika ili upate ufumbuzi na tusiruhusu majungu maeneo yetu ya kazi,” alisisitiza Mha. Saidy.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania