
Maafisa wa Marekani wanaohudhuria mazungumzo kati ya nchi hizo mbili mjini Berlin, Ujerumani, walisema jioni ya jana kwamba hakikisho hilo, hata hivyo, linapaswa kukubaliwa kwa haraka.
Wajumbe wa serikali ya Marekani kwenye mazungumzo hayo, Steve Witkoff na Jared Kushner, wanaripotiwa kusema kwamba asilimia 90 ya mpango wa amani imekubaliwa na pande husika, na kwamba sasa wanatazamia kumalizia sehemu iliyobakia.
Hata hivyo, viongozi wa Ulaya wamelipokea pendekezo kwa hadhari licha ya kusifia hatua zilizopigwa kwenye mkutano huo wa Berlin.
Ukraine bado inasuasua kwenye kukubali pendekezo la Marekani la kuachia sehemu ya ardhi yake mikononi mwa Urusi ili kukomesha vita hivyo.