Bunge la Zambia limepasisha kwa wingi wa kura mswaada wa kurekebisha vifungu vya katiba vinavyohusiana na uchaguzi ambavyo upinzani unadai vitamsaidia Rais Hakainde Hichilema katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Baada ya kura hiyo iliyoungwa mkono na wabunge 131 na kupingwa na wawili, waziri wa sheria Princess Kasune alisema kuwa hayo ni maagano na watu wa Zambia katika juhudi za kukuza haki na demokrasia.

Mbunge Francis Kapyanga kutoka chama cha upinzani cha Patriotic Front (PF) amesema “hatahalalisha kitu kisicho halali”.

Wanasiasa wa upinzani, mashirika ya kiraia na makundi ya makanisa yalikuwa yamepigia debe kupingwa kwa muswada huo nambari 7 na kusema uliharakishwa kupitishwa bungeni.

Mswaada huo pia ulitaka kufanyia marekebisho vifungu vya katiba ya taifa hilo la kusini mwa Afrika lenye utajiri wa shaba hasa kwa kuongeza idadi ya viti vya wabunge maalumu pamoja na kutenga viti 40 kwa wanawake, vijana na walemavu, na kuhitimisha ukomo wa mihula miwili ya miaka mitano kwa mameya.

Mswaada huo unapaswa kusainiwa na Rais Hichilema kuwa sheria.

Hakainde Hichilema Rais wa sasa ambaye ni kiongozi wa zamani wa Zambia mwaka 2021 aliibuka mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika, akimuangusha rais wa wakati huo Edgar Lungu.

Hichilema ameapa kutokomeza ufisadi nchini Zambia, hata hivyo wakosoaji wanasema kuwa maendeleo nchini humo yanasuasua.

Zaidi ya asilimia 64 ya wakazi wa Zambia, nchi yenye utajiri wa madini ya shaba, wanaishi katika hali ya umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *